BALANCE DIET
Sunday, 4 February 2018
Thursday, 25 January 2018
UMUHIMU WA BALANCE DIET
Kuna faida nyingi za kupata kula chakula bora, chache kati yake ni hizi:
Chanzo cha virutubisho
Kupata chakula bora kunaupa mwili virutubisho muhimu kwa afya na kujilinda na magonjwa. Mwili una uwezo wa kutengeneza virutubisho vingi, lakini kuna baadhi lazima vipatikane kutokana na chakula.
Kupungua uzito
Kuwa na uwiano mzuri kati ya mwili na uzito (au Body-Mass-Index BMI) ni kitu muhimu katika kuhakikisha afya yako iko sawa. Ukila chakula bora unahakikisha unapata virutubisho muhimu ili kuupa mwili wako uwezo wa kujiweka sawa na kutoongezeka uzito bila sababu.
Kuboresha kinga ya mwili
Mwili hufanya kila kitu kutokana na virutubisho vinavyopatikana. Kula chakula bora huupa mwili kiwango kizuri cha virutubisho vinavyohitajika ili kuimarisha mfumo wa kinga dhidi ya magonjwa.
Kuusaidia mwili kujijenga vizuri
Chukulia chakula kama dawa za kuutibu mwili. Chakula kizuri huupa mwili virutubisho vizuri ziadi na kuufanya uwe bora. Seli za mwili hujengeka kutokana na virutubisho vinavyopatikana kwenye chakula. Kukoseakana kwa aina fulani ya virutubisho hufanya seli za mwili kuwa dhoofu hivyo kutokuwa na siha njema.
VYAKULA SITA MUHIMU VYA BALANCE DIET
Kuna makundi sita ya vyakula, nayo ni Wanga (1.5%), mafuta (14%), protini (17%), madini (6%), vitamini (chini ya 1%) na maji (61%).
Miili yetu inapata nguvu kutoka kwenye makundi matatu ya vyakula – wanga, protini na mafuta. Tunahitaji hivi vyakula ili kuweza kuupa mwili nguvu na kuendelea kufanya kazi. Zingatia pia, miili yetu ina kiwango kikubwa sana maji, hivyo maji ni muhimu sana.
Wanga
Vyakula vya wanga vinatakiwa kuwa theluthi (1/3) ya kila mlo wako. Hii inamaanisha vyakula vyetu vingi vinatakiwa kuwa wanga. Baadhi ya vyakula vilivyo na wanga ni : viazi, vyakula vya nafaka (mchele, mahindi, mtama) na vinginevyo.
Protini
Protini ni muhimu kuufanya mwili kukua na kutengeneza seli zilizoharibika. Ni muhimu kula vyakula vilivyo na protini kwa wingi katika milo yako. Vyakula vyenye protini ni kama samaki, nyama, maharage na mayai. Protini pia hupatikana kwenye matunda na mboga mboga.
Madini na vitamin
Madini na vitamini ni virutubisho vinavyohitajika kwa kiasi kidogo mwilini, lakini ni muhimu sana kwasababu ya kazi yake inayofanya. Madini hutumika zaidi katika kujenga na kuboresha mifupa. Vitamini husaidia kwenye kazi muhimu tofauti mwilini. Vyakula vyenye madini na vitamini kwa wingi ni matunda na mboga za majani.
Mafuta na Sukari
Mafuta na sukari ni makundi mengine muhimu ya vyakula lakini yanatakiwa kuliwa kwa kiasi kidogo. Vyakula hivi vinaupa mwili nguvu nyingi sana. Kuzidisha kula vyakula hivi huufanya mwili kuhifadhi hivi vyakula na kumfanya mtu anenepe.
Unashauriwa kutumia zaidi mafuta yatokanayo na mimea na viumbe wa baharini tofauti na yale yanayotokana na wanyama na viwandani. Mafuta ya samaki huwa na omega fatty acids ambazo ni muhimu katika kukuza ubongo. Mafuta mabaya huufanya mwili ushindwe kushamiri na hivyo kupata matatizo zaidi.
Chakula bora hutakiwa kuwa na kiwango sahihi cha virutubisho hivi kama ilivyoainishwa hapo juu. Ila hakikisha kila mlo unapata matunda na mboga za majani, maana ni chanzo kizuri cha virutubisho asilia na vyenye faida zaidi mwilini mwako
FAHAMU KUHUSU BALANCE DIET
Balance Diet: Ni kula chakula cha kutosha na chakula kinachofaa ili kusaidia mwili kukua vyema, wa afya na kupigana na magonjwa.
Katika maeneo mengi duniani, watu wengi hula chakula aina moja ambacho hakina gharama ya juu karibu kwa kila mlo. Yaweza kuwa wali, mahindi, mtama, ngano, mihogo, viazi, shelisheli, au ndizi, hii ni kulingana na eneo alikotoka mtu. Chakula hiki kikuu kwa kawaida hupatia mwili chakula ambacho mwili unahitaji kila siku.
Hata hivyo, chakula hiki hakitoshi kupatia mtu afya. Chakula kingine cha kusaidia kinahitajika (kinacho saidia kwa ujenzi wa mwili). Vitamini na Madini (zinazo saidia kwa kulinda na Kukarabati mwili), na mafuta na sukari (ambazo humpa binadamu nguvu).
Lishe bora huwa na chakula tofauti, hii ni pamoja na chakula cha protini, matunda and mboga zilizo jaa vitamini na madini. Unahitaji kiwango kidogo cha mafuta na sukari. Lakini kama una shida ya kupata chakula cha kutosha, ni vyema ule chakula kilicho na sukari na mafuta kuliko kula chakula kidogo.
Mama hahitaji kula kila aina ya chakula kilichoorodheshwa hapa ili awe na afya. Anaweza kula chakula alichozoea na aongeze vyakula saidizi ambavyo vinapatikana katika eneo lake.
Subscribe to:
Posts (Atom)